Wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo wakiwa bungeni wamekubaliana kwa kauli moja kuwa posho za kila mbunge kwa siku ya leo zipelekwe kwa wazazi wa wanafunzi waliofariki kwa ajali ya basi la Shule ya awali na Msingi ya Lucky Vincent.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameongoza waombolezaji mbalimbali kuaga miili 35 ya marehemu katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
Mbali na Makamu wa Rais pia viongozi mbalimbali wa Serikali wameshiriki zoezi la kuaga miili ya wanafunzi,walimu na dereva waliofariki kwa ajali Arusha.
Social Plugin