Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WANACHAMA 681 KUTOKA UMOJA WA VIJANA WA CCM VYUO NA VYUO VIKUU WATUNUKIWA VYETI KWA KUHITIMU MASOMO YAO

Naibu Katibu Mkuu CCM Bara Ndg:Rodrick Mpogolo akisalimiana na Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka Mara baada ya kuwasili katika Mahafali ya Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu UVCCM Mkoa wa Dar Es Salaam  katika Ukumbi wa King Solomon Kinondoni.
Naibu Katibu Mkuu CCM Bara Ndg:Rodrick Mpogolo akisalimiana na Kaimu Mwenyekiti Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam Asha Ferouz Mara baada ya kuwasili katika Mahafali ya Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu UVCCM Mkoa wa Dar Es Salaam Leo katika Ukumbi wa King Solomon Kinondoni.
Naibu Katibu Mkuu CCM Bara Ndg:Rodrick Mpogolo pamoja na Kaimu katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka wakiwasili Ukumbini.
Naibu Katibu Mkuu CCM Bara Ndg:Rodrick Mpogolo pamoja na Kaimu katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka wakiteta jambo.
Naibu Katibu Mkuu CCM Bara Ndg:Rodrick Mpogolo pamoja na Kaimu katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka wakifurahia jambo.
Meza Kuu wakiburudika na nyimbo ya CCM uku wa kionesha Ishara Mshikamano na Umoja

Wahitimu wa Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu Wakicheza uku wa kishikana Mikono ishara ya Umoja
Wanafunzi wakishangilia
Kaimu Mwenyekiti wa Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam Asha Ferous akisoma Taarifa kwa Mgeni Rasmi Katika Sherehe za Mahafali ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Dar es Salaam Leo
Wana Vyuo na Vyuo Vikuu Wakiwa Ukumbini
Kaimu Katibu Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu UVCCM Taifa Ndg Daniel Zenda akizungumza katika Sherehe za Mahafali ya kuwaaga Makada wa CCM idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu uvccm Mkoa wa Dar es Salaam katika Ukumbi wa King Solomon Leo
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka akizungumza katika Sherehe za Mahafali ya kuwaaga Makada wa CCM idara ya Vyuo na
Vyuo Vikuu uvccm Mkoa wa Dar es Salaam katika Ukumbi wa King Solomon Kinondoni Leo
Baadhi ya Wahitimu wakimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka

Naibu Katibu Mkuu CCM Bara Ndg:Rodrick Mpogolo akipeana Mkono na Kaimu Katibu Mkuu UVCCM mara ya Baada ya kumaliza kuzungumza katika Sherehe za Mahafali ya kuwaaga Makada wa CCM idara ya Vyuo na
Vyuo Vikuu uvccm Mkoa wa Dar es Salaam katika Ukumbi wa King Solomon Kinondoni Leo
Wanavyunzi wahitimu Wakiimba Shairi katika Sherehe za Mahafali ya kuwaaga Makada wa CCM idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu uvccm Mkoa wa Dar es Salaam katika Ukumbi wa King Solomon Kinondoni Leo
Rais wa Serikali ya Wanafunzi Chuo Cha Kidemokrasia wa kwanza kulia Ndg:Aloyce Mukami akiwa katika mahafali hayo
Waziri Mkuu wa Serikali ya Wanafunzi Chuo Cha Madaktari MUHIMBILI akishangilia jambo katika Sherehe za Mahafali ya kuwaaga Makada wa CCM idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu uvccm Mkoa wa Dar es Salaam katika Ukumbi wa King Solomon Kinondoni Leo
Naibu Katibu Mkuu CCM Bara ndg:Rodrick Mpogolo akitoa Vyeti kwa Wahitimu Makada wa CCM Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam katika Sherehe za Mahafali ya kuwaaga Makada wa CCM idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu uvccm Mkoa wa Dar es Salaam katika Ukumbi wa King Solomon Kinondoni Leo
Kada Aldelatus Mushumbusi toka Tawi Idara ya Vyuo na Vyuo vikuu UVCCM Mabibo Hostel akikabidhiwa Cheti na Mgeni Rasmi Ndg :Rodrick Mpogolo katika Sherehe za Mahafali ya kuwaaga Makada wa CCM idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu uvccm Mkoa wa Dar es Salaam katika Ukumbi wa King Solomon Kinondoni Leo
Kada Aldelatus Mushumbusi toka Tawi Idara ya Vyuo na Vyuo vikuu UVCCM
Mabibo Hostel akipewa Mkono wa Pongezi na Ndg:Kaimu Katibu Mkuu Uvccm Shaka Hamdu Shaka katika Sherehe za Mahafali ya kuwaaga Makada wa CCM idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu uvccm Mkoa wa Dar es Salaam katika Ukumbi wa King Solomon Kinondoni jana 
Kaimu Mwenyekiti wa Idara ya Vyuo na Vyuo vikuu UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam Asha Ferouz akikabidhiwa Cheti cha pongezi na Mgeni Rasmi ndg:Rodrick Mpogolo katika Sherehe za Mahafali ya kuwaaga Makada wa CCM idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu uvccm Mkoa wa Dar es Salaam katika Ukumbi wa King Solomon Kinondoni jana.
“Ujana ni rika, ujana ni wakati na wakati haurudi
nyuma” haya yalizungumzwa na mgeni rasmi Ndg. Rodrick Mpogoro Naibu katibu Mkuu CCM Bara kwenye mahafali ya Vijana Chama Cha mapinduzi kutoka Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Dar es Salaam yaliyofanyika leo 28/05/2017 katika ukumbi wa King Solomoni Kinondoni. 

Ndg. Rodrick Mpogoro alisema, Siri pekee ya kufanikiwa kwa mtu yeyoteinategemea namna anavyotazama na kutathmini mambo. 

Ni mtazamo chanya pekee ndiyo humvusha mtu kwenye mafanikio, hivyo ipo haja kwenu vijana kujikita kutazama fursa zinazowazunguka na kuwa wabunifu ili
kujitengenezea vipato vyenu wenyewe kuliko kusubiria ajira, alisema.

“Sura ya Chama Cha Mapinduzi inajengwa na wanachama wenyewe kwa vitendo,jengeni uadilifu, zungumzeni habari ya uzalendo wa nchi yenu, jengeni maslahi kwa wanyonge, jifunzeni historia ya Chama, someni katiba na kanuni zake, fanyeni kazi kwa bidii na jengeni moyo wa kujitolea
mkifanya hayo mtafanikiwa*. Alisema.

Alifahamisha kuwa ni vyema kwa wanachama, wananchi na kila mpenda amani, umoja na maendeleo ya Taifa kuendelea kumuunga mkono Rais wetu Mhe Dr. John Pombe Magufuli katika juhudi anazozifanya za kupambana na ubadhilifu wa mali za umma kwani anaiishi misingi ya Chama Cha mapinduzi kama ilivyoainishwa kwenye madhumuni yake kupitia katiba Ibara ya 5. 


*”Simameni imara katika kumuunga mkono Rais wetu kwani anaiishi misingi ya Chama Cha Mapinduzi katika kujenga uzalendo wa nchi”.
Mgeni Rasmi Naibu Katibu Mkuu CCM Bara Ndg Rodrick Mpogolo akizungumza na Wahitimu Makada wa CCM Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu UVCCM katika Sherehe za Mahafali ya kuwaaga Makada wa CCM idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu uvccm Mkoa wa Dar es Salaam katika Ukumbi wa King Solomon Kinondoni Leo
Maonyesho ya karatee
PICHA ZOTE NA FAHADI SIRAJI UVCCM

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com