Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WAZIRI WA AFYA AELEZA HALI YA UGONJWA WA EBOLA TANZANIA

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Ally Mwalimu amesema mpaka sasa hakuna mgonjwa wa Ebola wala anayehisiwa kuwa na virusi vya ugonjwa huo nchini Tanzania huku Tsh. bilion 1.5 zikiwa zimetumika kuukabili ugonjwa huo

Ummy amebainisha hayo leo wakati alipokuwa anazungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam na kusema wananchi wasiwe na hofu ila wanapaswa kuchukua tahadhari huku akisisitiza kuwa wameweka kifaa maalum 'register' ambacho kitawalazimu wasafiri wote kujaza wakiwa wanakwenda katika nchi ya DRC na pindi wakiwa wanatoka huko kuingia nchini.


"Hadi sasa hakuna mgonjwa hata mmoja wa Ebola wala mwenye virusi Tanzania, tumechukua tahadhari katika mikoa yote inayopakana na nchi ya Congo DRC. Wasafiri wote wanaotoka DRC wakifika Tanzania lazima waandikishwe kimaalum ili kufuatiliwe kama huko alikotoka hali ikoje na kama hana virusi nyemelezi. Tunawaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza katika kuwapima wasafiri wote kwenye mipaka yetu na Congo DRC" alisema Ummy.


Aidha, Ummy amesema serikali imeagiza mashine nne za nyongeza kutoka nje ya nchi ili kuongeza nguvu ya upimaji wa virusi vya ugonjwa huo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com