Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WIZI WA PUNDA TISHIO KENYA...WEZI WANACHUKUA NGOZI TU


CITIZEN TV ya Kenya imeripoti taarifa ya wizi wa punda uliokithiri huko Turkana kiasi kwamba hata Wakazi wenyewe wamejawa na hofu na kisa kikiwa ni kuuzwa kwa ngozi ya punda hao.

Biashara ya kuuzwa ngozi ya punda inadaiwa kuwa imeletwa na Wachina na kufanya ngozi ya mnyama huyo kupanda thamani hadi shilingi za Kenya 10,000 ambazo ni zaidi ya shilingi laki mbili za Tanzania huku Punda mwenyewe akiuzwa Ksh 5000 (laki moja na elfu nane ya Tanzania).

Wanasema baada ya Wachina kuinunua ngozi hiyo husafirishwa na kwenda kutumika kwenye kutengeneza dawa inayotibu magonjwa mbalimbali kwenye mwili wa binadamu.

...>>>”Unaweza nunua punda kwa elfu 5 au sita na ukauza ngozi kwa Elfu 10 hali hiyo ikaleta thamani ya Punda na ndiomaana wezi wanaiba Punda na kumchuna ngozi ili aje auze ngozi peke yake” – Joseph Losuru 

“Tuliona kwenye media za Nigeria kuwa Punda wameisha lakini na hapa kwetu pia Punda wameanza kuisha” – Lokwale Anton Mfugaji

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com