AKAMATWA NA TAKUKURU AKIJIFANYA MHANDISI WA JIJI LA MWANZA ALAMBE RUSHWA YA LAKI 2


James Edward
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ‘TAKUKURU’ imemkamata mtu aliyekuwa anajifanya Mhandisi wa Jiji kisha kuomba rushwa.


Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Mwanza, Erenst Makale amesema mtu mmoja anayefahamika kwa jina la James Edward ambaye ni Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Mtakuja amekamatwa na Taasisi hiyo kwa kujifanya Mhandisi wa Jiji kisha kuomba rushwa ya Tsh. 200,000 kwa Mfanyabiashara.


"Mtumishi huyu aliomba kwa Mfanyabiashara wa Zana za Kilimo ambaye Zana zake aliweka kwenye eneo ambalo ni Hifadhi ya Barabara…huyu mtu aka-take advantage (faida) akaenda kwake akijitambulisha kama Mhandisi wa Jiji.
 Akamtaka aondoe Zana zake za Kilimo au ampe Shilingi Milioni Moja. Katika kujadiliana, wakajadiliana wakashusha mpaka kwenye Laki Mbili.


"Mwananchi huyu akawa Muungwana akaja Ofisini kwetu. Tukafanya mtego tarehe 13, mtego huo ukafanikiwa lakini hela ilienda kupokelewa na Bwana Godfrey Joseph Mwangonda ambaye ni Afisa Mtendaji wa Kata ya Mkolani. Mtu ambaye aliomba fedha ni Bwana James Edward Mwasemela ambaye ndiye Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Mtakuja.


"Baada ya kumkamata tulikuja kubaini vitu vingine vya zaida kwamba mtu huyu James Edward Mwasemela ni sugu pamoja kwamba ni Mtumishi wa Umma lakini ameshiriki tena kwenye makosa mengine ya utapeli na kufunguliwa kesi mbili katika mwaka 2013 na 2016 na baadaye kesi hizo ziliondolewa…” Amesema Erenst Makale.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم