Mbunge wa Nkasi (CCM), Ally Kessy amefunguka na kusema watu waliohusika kusaini mikataba mibovu ya madini wanatakiwa kunyongwa kwani nchi ikitapoteza watu ishirini au thelathini hakuna hasara yoyote.
Mbunge Kessy anasema kama watu hao waliotia saini ya mikataba ya madini mwaka 1998 watakamatwa na mali zao kunyang'anywa na wakanyongwa itakuwa ni fundisho kubwa kwa watu wengine na baadhi ya wabunge wengine waliunga mkono hoja hiyo huku wakitaka mikataba hiyo ya madini iweze kupitiwa upya.
"Wakamatwe wote waliohusika na mikataba mibovu na kusababisha kuingizia serikali hasara, ikiwezekana wanyongwe hata ishirini au thelathini maana nchi hii wanazaliwa watu Muhimbili zaidi ya mia moja kwa siku, Bungando wanazaliwa mpaka Namanyele wanazaliwa kwa hiyo tukipoteza watu mia moja au mia mbili Mh. Spika hakuna kitu kitakachopotea katika nchi hii, tumeonewa vya kutosha haiwezekani"alisisitiza Ally Kessy na kuongeza;
"Mnasema mnarekebisha mikataba, mikataba kurekebisha ni kutafuta hao wote waliosaini wakamatwe, wanyang'anywe mali zao, wanyongwe tutabaki salama katika hii nchi, itakuwa mfano, nataka comment ya serikali kusikia kuwa tutashughulikia wote waliotia saini mikataba ya madini 1998 wakamatwe mara moja" alisema Kessy
Social Plugin