WAKATI mkoa wa Arusha ukiwa na upungufu wa walimu 788 sawa na asilimia 58.85 ya mahitaji ya walimu mkoani hapa, imebainika kuwa, walimu 261 wamebainika kuwa na vyeti feki.
Mkoa wa Arusha wenye shule za sekondari za serikali 162, una upungufu wa walimu 197 wa Fizikia, 243 wa Kemia, 85 wa Bayolojia na 263 wa hisabati. Kwa mujibu wa Ofisa Elimu-Taaluma wa mkoa wa Arusha, Eugene Shirima kazi ya kubaini walimu wenye vyeti feki mkoani humo imethibitisha kuwepo na walimu 261 vyenye vyeti feki hadi sasa wakiwemo walimu wa masomo ya sayansi na baadhi yao wamelazimika kujiondoa kazini.
Hata hivyo, Shirima amefafanua baadhi ya walimu wamelazimika kukata rufaa Baraza la Mitihani la Taifa na Idara ya Utumishi kupinga hatua ya kuwaondoa kazini. Amesema mbali na walimu hao kubainika kuwa na vyeti feki baadhi ya walimu wamelazimika kujiondoa wenyewe bila hata kutoa taarifa kwa mwajiri wao katika halmashauri za wilaya ama kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha.
Via>>Habarileo
Social Plugin