Mwanamme mmoja aliyefahamika kwa jina la Pius Luteko(42) mkazi wa kijiji cha Nankanga A tarafa ya Kipeta wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa ameuawa kwa kukatwa mapanga baada ya kufumaniwa akifanya mapenzi kwenye pagala (nyumba ambayo haijamalizika kujengwa) na mke wa mtu.Mwandishi wa Malunde1 blog Walter Mguluchuma anaripoti.
Tukio la kuuawa mtu huyo limetokea Juni 5, mwaka huu majira ya saa 11:40 ambapo watuhumiwa watatu walimvizia mtu huyo na kufanikiwa kumkuta Luteko na mwanamke huyo katika pagala na ndipo walipomkata mapanga kisogoni na kumsababishia kifo papo hapo.
Kamanda wa polisi mkoa wa Rukwa George Kyando alisema baada ya kufanya mauaji hayo mmoja kati ya watu waliofanya mauaji alifanikiwa kukimbia na serikali ya kijiji iliwakamata watuhumiwa wawili akiwemo mume wa mwanamke huyo na kuwafikisha polisi na wanashikiliwa mpaka hivi sasa.
Aidha kamanda Kyando alisema siku ya Juni 6 majira ya 11:45 huko katika kijiji cha Mpansa, kata ya Mpalamawe,tarafa ya Namanyere, wilaya ya Nkasi kulitokea ajali ya gari lenye namba za usajili STL 3634 Landcruiser deffender mali ya TASAF Mkoa wa Rukwa.
Gari hilo lilikuwa likiendeshemwa na dereva Saad Yazid(55) mkazi wa Sumbawanga, liliacha njia na kupinduka na kusababisha majeruhi kwa James Kapenulo( 37) Afisa Takwimu katika ofisi ya mkuu wa mkoa huo, Aziza Kalyatila(38) Afisa Ustawi wa Jamii katika ofisi ya mkuu wa mkoa pamoja na dereva wa gari hilo ambaye ni mtumishi katika ofisi ya mkuu wa mkoa pamoja na kusababisha uharibifu wa gari.
Kamanda huyo wa polisi alisema chanzo cha gari hilo kupinduka ni kuacha njia kutokana na mwendo kasi wa dereva.
Alisema majeruhi hao wapo hospitali ya mkoa Sumbawanga kwa matbabu na mtuhumiwa amekamtwa ingawa naye ni mmoja wapo kati ya majeruhi atafikishwa mahakamani pindi atakapopata nafuu.
Katika tukio la mwisho likilotokea pia Juni 6 majira ya saa 01:00 jioni huko katika kijiji na kata ya Ulumi tarafa ya Uwimbi Wilaya ya Kalambo Mkoa wa Rukwa pikipiki yenye namba MC 449 ATE aina ya sunlg Iliyokuwa ikiendeshwa na Emanuel NtanduMfipa(40) mkazi wa Kazonzya aligongana na mpanda baiskeli, Aitwaye Aidan Mkata Mfipa(17) Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Mambwe Mkazi wa Ulumi na kumsababishia majeraha ambapo baada ya kugongwa alivunjika mkono wa kulia.
Aidha katika ajali hiyo mwendesha bodaboda naye alipata majeraha kifuani na wote wamelazwa katika kituo cha afya Mwimbi.
Chanzo cha ajali ni mwendokasi wa mwendesha pikipiki ambaye pia ni mmojapo wapo wa majeruhi na amekamatwa na atafikishwa mahakamani baada ya kupata nafuu.
Na Walter Mguluchuma- Malunde1 blog Sumbawanga
Social Plugin