Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Balaa Kahama!! MSAKO WA WAENDESHA BODABODA WAPATA MIILI YA WATU WALIOUAWA NA KUTUPWA...WACHOMA MOTO MASHAMBA,SHUHUDIA HAPA


Watu wawili wanaosadikiwa kuwa ni madereva bodaboda wa mjini Kahama wamekutwa wakiwa wamekufa katika Shamba la miti linalomilikiwa na mkulima, Marco Nkuli katika eneo la Nyakato wilayani Kahama mkoani Shinyanga.



Watu hao ambao majina yao hayakufahamika mara moja, wamekutwa katika eneo hilo kufuatia msako uliofanywa na madereva bodaboda katika mashamba hayo wakimtafuta dereva mwenzao aliyekuwa amepotea na kukutwa ameuawa kwenye msitu huo mwishoni mwa wiki iliyopita.


Baada ya kukuta miili hiyo waendesha bodaboda wameamua kuchukua uamuzi wa kuteketeza kwa moto mashamba ambako miili hiyo imekutwa.

Baadhi ya madereva bodaboda wamesema kuwa miili hiyo imekutwa ikiwa na majeraha sehemu mbali mbali huku viungo vingine vya binadamu likiwemo fuvu la kichwa eneo vikiwa katika eneo hilo.

Wakiongea mbele ya ofisi ya mkuu wa wilaya, Madereva hao wameiomba serikali kumnyang’anya mmiliki huyo eneo hilo kwani limekuwa likitumika kama kichaka cha kujifichia wahalifu wanaowateka na kuwaua madereva bodaboda na kuchukua pikipiki zao.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida madereva hao wamevamia na kuchoma moto mashamba hayo ya miti yanayokadiriwa kuwa na ukubwa wa heka 50 huku wakisema kuwa uamuzi huo umelenga kusafisha eneo hilo ambalo linadaiwa kuficha wahalifu.

Nao baadhi ya majirani wanaoishi kuzunguka mashamba hayo wamepongeza uamuzi huo wa madereva boda boda kuchoma eneo hilo, na kuongeza kuwa wamekuwa wakiishi kwa hofu kutokana na uwepo wa vichaka hivyo.

Kwa upande wake mkuu wa kitengo cha upelelezi Polisi Kahama, George Bagemu amesema watuhumiwa watatu wa mauaji hayo wamekamatwa Kakonko mkoani Kigoma na watasafirishwa kuletwa Kahama kwa ajili ya hatua zaidi za upelelezi.

Tukio hilo linajiri wakati ambapo kumekuwa na ongezeko la matukio ya kutekwa kwa madereva bodaboda na pikipiki zao kuibiwa wilayani Kahama.

Mafisa wa polisi wakishusha miili ya madereva boda boda na fuvu la kichwa ili kuhifadhiwa katika chumba cha maiti katika hospitali ya wilaya ya Kahama.
Zoezi la kushusha miili hiyo likiendelea
Miili ya watu wanaodaiwa kuwa waendesha boda boda iliyokutwa katika msitu wa Mwanankuli ikiingizwa mochwari.
Madereva boda boda wakiwa katika ofisi ya mkuu wa wilaya ya Kahama wakihitaji kuongea na mkuu wa wilaya kuhusu eneo la msitu wa Mwanankuli.
Huduma za usafiri wa boda boda nazo zikasimama kwa muda baada ya madereva boda boda kuandamana wakihitaji kuongea na mkuu wa wilaya.
Afisa wa polisi akiwasihi madereva boda boda waliokuwa nje ya geti la mochwari kutulia wakati suala lao likifanyiwa kazi.
Madereva boda boda wakiwa nje ya geti kuu la hospitali ya wilaya ya Kahama.
Eneo la mashamba ya Mwana Nkuli Nyakato likiteketea kwa moto baada ya madereva boda boda kulichoma.
Mashamba hayo yakiendelea kuteketea kwa moto
Moto ukiendelea kusambaa
Moto ushamaliza kazi yake kwenye mashamba ya Mwana Nkuli
Askari wa kikosi cha zima moto na uokoaji wakiuzima moto uliokuwa unaelekea katika shule ya Sunset.
Shule ya msingi Sun set ambayo iko karibu na msitu huo,ambapo moto ulikwa umeaanza kuifikia.
Gari la zima moto kutoka Mgodi wa Buzwagi likitoa msaada wa kuzima moto katika eneo la shule ya Sunset.
Askari wa kikosi cha zima moto na uokoaji wakiendelea kuzima moto.
Picha zote na Mwandishi wa Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com