Habari tulizozipata hivi punde ni kwamba basi la Wibonela Express lenye namba za usajili T158 CEX lililokuwa linatoka Dar es salaam kuelekea Kahama mkoani Shinyanga limegongana
na basi la Tak-biir lenye namba za usajili T818 CYQ katika eneo la Kibaigwa mkoani Dodoma ambapo ujenzi wa
barabara unaendelea.
Taarifa zinasema hakuna abiria aliyepoteza maisha lakini watu kadhaa wamejeruhiwa.
Baadhi ya abiria waliokuwa kwenye basi la Wibonela wanasema chanzo cha ajali hiyo ni dereva wao ambaye alikuwa anaendesha basi kwa mwendo kasi na hakujali malalamiko ya abiria wake kila walipomwambia apunguze mwendo.
"Hii ni mara ya pili,ya kwanza tulinusurika kupata ajali,alikuwa anaovatek 'anajaribu kuyapita magari mengini' bila kuchukua tahadhari,ukiwaambia wanakuwa wabishi",wamesema.

Social Plugin