Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) umemtia mbaroni kijana mmoja aliyekuwa akijifanya daktari na alikuwa akijitambulisha kwa wagonjwa kwa jina la Dkt. Abdallah Juma.
Aidha, kijana huyo alijifanya kutoa huduma katika maabara kuu ya Hospitali hiyo huku uongozi ukiwa hauna taarifa ya kuwepo kwa huduma aliyokuwa akiitoa kitu ambacho kilisababisha kushtukiwa na kukamatwa.
Baada ya kukamatwa Uongozi wa hospitali hiyo ulifanya uchunguzi na kubaini kuwa kijana huyo hakuwa daktari bali daktari feki kama alivyokuwa akijitambulisha na kwamba amekamatwa mara baada ya kuwekewa mtego na askari wa hospitali hiyo.
Hata hivyo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Wateja wa Hospitali hiyo, Aminiel Aligaesha amesema hospitali imeweka mikakati mbalimbali ya kupambana na wahalifu wakiwamo watu wanaojiita ni madaktari kama huyo ambaye alikamatwa jana.