Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

DEREVA ATAKAYESABABISHA AJALI TANZANIA KUCHARAZWA VIBOKO




BARAZA la Taifa la usalama barabarani limeadhmia kuanza mpango mkakati wa awamu ya pili ambao katika utekelezaji wake pamoja na mambo mengine 12, utahusisha kuwachapa viboko madereva watakaokiuka sheria za usalama barabarani.

Hayo yameelezwa mjini Dodoma na mwenyekiti wa baraza hilo ambaye pia Naibu Waziri wa mambo ya ndani Mhandisi Hamad Yusuf Massauni (pichani) wakati akitoa taarifa ya tathmini ya utekelezaji wa mpango wa mkakati wa kupunguza ajali barabani nchini kwa asilimia 10 katika kipindi cha miezi sita kuanzia Agosti 2016 hadi Januari 2017.

Amesema baada ya kuona kuwa utelekezaji wa awamu ya kwanza umefanikiwa kwa kiasi kukubwa kupunguza ajali baraza hilo limeamua kuanzishe awamu ya pili ambapo moja ya mikakati yake itawachukia hatua kali wale wote watakaokiuka sheria hizo.

Hata hivyo Baraza hilo liliundwa kwa mujibu wa sheria ya usalama barabarani sura ya 168 kama ilivyorejewa mwaka 2002 ambapo lengo kubwa ni kuratibu, kueleimisha, kushauri,kuelekeza, kuunganisha wadau mbalimbali wa usamala barabarani.


Mbali na kuyabainisha mambo 12 ambayo watayazingatia katika awamu ya pili, hapa mwenyekiti huyo anabainisha baadhi ya mambo hayo.

Akizungumzia operesheni,usimamizi wa sheria na hatua zilizofikiwa katika kipindi hicho cha miezi sita katika awamu ya kwanza, amesema jumla ya madereva 1596 walikamatwa, kuwekwa mahabusu na kupelekwa mahakani badala ya kulipa faini ya papo kwa papo kama walivyokuwa wamezoea.

Amesema kuwa magari 188,602 yalikamatwa kutokana na ubovu ambapo kati ya hayo magari 623 yalifungiwa kutembea kutokana na ubovu.

Kuhusu athari zilizotolewa katika kipindi hicho cha awamu ya kwanza, Mhandisi Massauni amesema kuwa jumla ya askari 117 ambao hawakufanya vizuri katika utekelezaji wa mpango huo walichukuliwa hatua mbalimbali za kinidhamu.

Mhandisi Massauni amewataka watanzania kuhakikisha kuwa wanazingatia sheria za usalama barabarani pamoja na kuzingatia kaulimbiu isemayo “hatutaki ajali tunataka kuishi salama.

Na Josephine Charles-Malunde1 blog Dodoma

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com