Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

News Alert: POLISI WAPIGA MABOMU YA MACHOZI,MAJI YA KUWASHA KUTAWANYA WAENDESHA BODABODA SAKATA LA KIFO CHA MWENZAO SHINYANGA


malunde1 blog

Askari polisi akipiga bomu nyumbani kwa marehemu mwendesha bodaboda kusambaratisha waombolezaji leo Shinyanga-Picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog

Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limetumia mabomu ya machozi na maji ya kuwasha kuwasambaratisha waendesha bodaboda mjini Shinyanga waliokuwa wamefunga barabara kuu ya Shinyanga – Tabora wakidai askari wa jeshi hilo amesababisha kifo cha mwendesha bodaboda mwenzao- SOMA HABARI KAMILI HAPA



Mabomu ya machozi yameanza kupigwa leo Jumatano June 7,2017 tangu asubuhi mpaka majira ya saa sita mchana  katika mitaa mbalimbali mjini Shinyanga.

Wakati polisi wakipiga mabomu,wananchi,waendesha bodaboda nao walikuwa wanajibu mashambulizi kwa kuwarushia mawe askari polisi.



Pamoja na jeshi hilo kupiga mabomu, limekwenda hadi nyumbani kwenye msiba alipokuwa akiishi marehemu na kuwatawanya kwa kuwakamata bodaboda na pikipiki zao hali iliyozua taharuki zaidi.



Inaelezwa kuwa waendesha bodaboda hao wamegoma kumzika mwenzao wakishinikiza mpaka mkuu wa mkoa afike nyumbani kwa marehemu.
SOMA HABARI KAMILI <<HAPA>>
malunde1 blog, vurugu shinyanga
Gari la maji ya kuwasha likimwaga maji 

malunde.com vurugu shinyanga,polisi waendesha bodaboda
Askari polisi wakiwa mtaani,kulia ni gari la kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga
www.malunde.com,vurugu shinyanga

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com