Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KUHUSU TAARIFA ZA KIFO CHA SHABIKI MAARUFU WA TIMU YA YANGA 'ALLY YANGA'



Shabiki maarufu wa timu ya Yanga Ally Mohamed almaarufu kwa jina la Ally Yanga.amefariki Dunia mapema leo katika ajali ya gari eneo la kijiji cha Chipogoro wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma. 

Kamanda wa polisi Mkoa wa Dodoma Lazaro Mambosasa amethibitisha kifo cha aliyekuwa shabiki maarufu wa klabu ya soka ya Yanga Ally Yanga kilichotokea leo katika ajali ya gari aina ya Rav4 eneo la Chipogolo wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma.

Ally Yanga ambaye pia ni mkereketwa wa Mwenge wa Uhuru alikutwa na mauti akiwa katika gari la kampuni ya Faidika ambalo lilikuwa kwenye shughuli zake za promosheni na SIO KWAMBA alikuwa kwenye msafara wa Mwenge kama inavyoenezwa.

Ally aliyezaliwa mkoani Shinyanga Machi 1, mwaka 1984 katika familia ya watoto sita, kabla ya umauti wake inafahamika alikuwa anaishi Yombo Vituka, Dar es Salaam.

Lakini tangu baada ya uchaguzi Mkuu Novemba 2015, Ally Yanga ameadimika viwanja vya soka kutokana na kujikita zaidi kwenye shughuli za Chama cha Mapinduzi CCM.
Pichani chini ni gari iliyosababisha kifo cha Shabiki huyo wa Yanga,Ally Yanga

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com