Mbunge wa Jimbo la Hai,Freeman Mbowe akiwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo Helga Mchomvu wakati wa Futari ya pamoja iliyoandaliwa na Mbunge huyo katika miskiti minne tofauti.
Baadhi ya Waumini wa Dini ya Kiislamu wakipata Futari katika msikiti wa Kibaoni wilayani Hai.
Sheikh Mkuu wa wilaya ya Hai,Omar Mohamoud akizungumza wakati wa hafla ya kupata Futari iliyoandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Hai,Freeman Mbowe.
Imamu wa Msikiti wa Kambi ya Nyuki ,Fahad Lema akisoma Risala kwa Mbunge wa jimbo la Hai,Freeman Mbowe mara baada ya kumalizika hafa ya kupaa futari kwa pamoja katika msikit wa Kibaoni wilayani humo.
Mbunge wa Jimbo la Hai,Freeman Mbowe akisalimiana na Imamu wa Msikiti wa Kambi ya Nyuki Fahad Lema mara baada ya kuwasilisha ombi la kusaidiwa ujenzi wa vyumba vya madrasa ambapo Mh Mbowe alichangia kiasi cha Sh Mil,2 kwa ajili ya kununua mbao za kuezekea Paa.
Mbunge wa jimbo la Hai,Freeman Mbowe akisalimana na Waumini katika Msikiti wa Kibaoni uliopo Bomang'ombe wilayani Hai ,mara baada ya kumalizika kwa hafla ya kupata futari iliyoandaliwa na Mbunge huyo katika miskiti minne tofauti katika jimbo hilo.
Mbunge wa jimbo la Hai,Freeman Mbowe akipata Futari na waumini wengine katika Msikiti wa Lambo uliopo Machame wilayani Hai baada ya kushiriki pia katika miskiti mingine mitatu .
Mmoja wa viongozi wa Dini ya Kiislamu Mwl Mohamed Mbowe akizungumza wakati akimkaribisha Mbunge wa jimbo la Hai,Freeman Mbowe katika Msikiti wa Lambo .
Mjumbe wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Alhaji ,Habib Nasiwa akikabidhi Cheti cha Heshima kwa Mbunge wa jimbo la Hai,Freeman Mbowe kwa jitihada zake za kuleta umoja katika Dini na Madhehebu mbalimbali katika wilaya hiyo.
Mbunge wa jimbo la Hai,Freeman Mbowe akionesha zawadi ya Cheti alichokabidhiwa na Waislamu katika wilaya ya Hai.
Mbunge wa jimbo la Hai,Freeman Mbowe akikabidhi zawadi ya Cheti kwa Diwani wa kata ya Machame Kaskazini,Clement Kwayu ili afungue na kusoma kilichoandikwa ndani.
Diwani wa kata ya Machame Kaskazini,Clement Kwayu (Mwenye suti) akisoma maneno yaliyoandikwa katika Cheti kilichotolewa na Waislamu wa wilaya ya Hai,kwa Mbunge wa jimbo hilo Freeman Mbowe.
Mbunge wa jimbo la Hai,Freeman Mbowe akishiriki Dua mara baada ya kumalizika kwa hafla ya Futari iliyoandaliwa katika misikiti minne tofauti ukiwemo msikiti wa Lambo uliopo Machame wilayani Hai.
Baadhi ya wauimini wa Dini ya Kiislamu wakiwasiliza viongozi mara bada ya kushiriki hafla ya Futari iliyoandaliwa na Mbunge wa jimbo la Hai,Freeman Mbowe.
Msikiti wa Lambo uliopo Machame ambao Mbunge wa jimbo la Hai,Freeman Mbowe amechangia kwa kiasi kikubwa ujenzi wake.
******
MBUNGE wa Jimbo la Hai na Kionozi wa Kambi rasmi Bungeni,Mh ,Freeman Mbowe ametunukiwa cheti cha heshima na jamii ya Waislamu katika wilaya ya Hai kutokana na jitihada zake zisizo na ukomo katika kuleta umoja katika Dini na Madhehebu mbalimbali.
“Tunaamini katka Uhuru wa kuabudu na kujieleza ,malumbano ya hoja na mijadala ,Kuvumiliana na kusamehe, Vitisho ,ugandamizaji na uonevu wa aina yoyote vinaweza kuendelea lakini havitaweza kushinda jamii yetu. Uhuru ni tunu ya sili tuliyopewa na Mwenyezi Mungu Mtukufu” yalieleza maeno yaliyopo katika Cheti hiycho.
Mh Mbowe alikabidhiwa cheti hicho na Mjumbe wa Baraza Kuu la Waisalmu (BAKWATA) Alhaji Habib Nasiwa , katika msikiti wa Lambo uliopo Machame wilayani muda mfupi baada ya kumalizika kwa hafla ya kushiriki futari iliyoandaliwa na mbunge huyo katika misikiti minne tofauti ya Modio ,Rundugai,Kibaoni na Lambo.
Cheti hicho kilichosainiwa na Sheakh Mkuu wa wilaya ya Hai,Sheakh ,Omary Mahmoud ambaye pia ni katibu wa msikiti wa Kibaboni Bomangombe kimetolewa ikiwa ni ni ishara ya kutambua mchango mkubwa unatolewa na Mbunge huo kwa Waislamu.
Akizingumza mara baada ya kukabidi cheti hMjumbe wa Baraza kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Alhaji Habib Nasiwa alitoa shukrani kwa niaba ya waislamu wa jimbo la Hai kwa namna ambavyo ameendelea kujitoa pamoja na kuchangia ujenzi wa msikiti wa Lambo.
“Nimehemewa sana ,sidhani kama naweza kusema kiasi cha kutoshereza ,nimehemewa na kujaaa furaha ya kufikiwa na Mh Mbowe,halikua jambo rahisi la kumpata leo ,kwanza tukijua Bunge linaendelea kadharika tukijua kwamba ana majukumu mengine mengi lakini akaona ashiriki na sisi wilaya ya Hai.”alisema Nasiwa.
“Jambo fupi la kukushirikisha jioni ya leo,mheshimwa tunakupongeza kwa kujua umuhimu wa ramadhan kwa kuacha shughuli zako na kuja kushiriki nasi katika kutufuturisha,tunakupa asante sana na mungu akubariki sana,”aliongeza Alhaji Nasiwa.
Katika hafla hiyo ya kufuturisha ,Mh Mbwe alishiriki katika misikiti yote minne ambapokatika msikiti wa Mudio alitoa mifuko 100 ya Saruji kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya msingi inayomilikiwa na msikiti huo na pia alikabidhi kiasi cha sh Mil moja kwa msikiti wa Rundugai kwa ajili ya mwalimu anayefundisha masomo ya dini katika shule ya Msingi na Sekondari za Rundugai .
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.