MKUU wa Wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro amelazimika kula chakula na kunywa maji yaliyotoka kwenye mradi wa maji wa kisima kirefu uliokataliwa na wananchi kwa hofu kuwa wakinywa maji hayo watakufa na wakipikia chakula kitabadilika rangi ya njano.
Mkuu huyo akiwa kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji hicho juzi alitaka kusikiliza kero za wananchi na kufahamu kwanini wanaendelea kutumia maji ambayo siyo safi na salama ikiwa mradi upo tangu mwaka 2014 hawajawahi kuyatumia.
Matiro aliyekuwa ameambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama na viongozi wengine na baada ya kusikiliza hoja hiyo walilazimika kuyaonja na kupika chakula kwa haraka na kubainika hayana chumvi wala chakula kilichopikwa kutokuwa cha njano ndipo ilipobainika kuwa walidanganywa kwa sababu za kisiasa.
IMEANDIKWA NA KAREN MASASY, SHINYANGA
Social Plugin