Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MWALIMU AJIUA KWA KUNYWA SUMU GESTI



Mwalimu  Betson Sanga aliyekuwa akifundisha Shule ya Sekondari Milundikwa  wilayani Nkasi   amefariki dunia baada ya kunywa sumu akiwa katika nyumba ya kulala wageni   mjini Sumbawanga.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, George Kyando alisema   mwalimu huyo alifariki dunia juzi usiku huku akiwa ndani ya chumba alichokuwa amepanga  karibu na kituo kikuu cha    mabasi yanayokwenda  mikoani.

Alisema hadi sasa   hajafahami chanzo cha mwalimu huyo kujiua kwa   sumu ingawa aliacha ujumbe uliosomeka, “Kama nadaiwa deni lolote na mtu amweleze mkurugenzi ambaye ni mwajiri wangu lakini asilaumiwe, nisilaumiwe chochote juu ya kifo change”.

Inadaiwa kwamba siku ya tukio mwalimu huyo  alifika katika nyumba hiyo ya kulala wageni na kupanga chumba kwa ajili ya kulala na baadaye  alikabidhi funguo na kuondoka kwenda kusikojulikana.

Taarifa zinadai   ilipofika usiku wa manane alirejea katika nyumba hiyo akiwa amelewa akachukua ufunguo kwa mhudumu  na kuingia ndani ya chumba chake   kulala.

Baada ya muda mhudumu wa nyumba hiyo alisikia sauti ya mtu akikoroma kwa sauti ya juu hali iliyzua hofu.

Mhudumu   alilazimika kuomba msaada kwa wapangaji wengine waliokuwamo ndani ya nyumba  hiyo na  kuvunja mlango.

Baada ya kuvunjwa kwa mlango mhudumu huyo akiwa na wapangaji hao, walimkuta mwalimu huyo akiwa anatokwa mapovu hali iliyowalazimu kumkimbiza  hospitalini lakini wakiwa njiani alifariki dunia.

RPC Kyando  alisema kwa mujibu wa uchunguzi wa utabibu,   Mwalimu  Sanga alikunywa sumu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com