Dola za Marekani
Mtu mmoja kusini mwa Msumbiji katika mkoa wa Inhambane alilazimika kumlipia mahari mkewe aliyefariki wikiendi iliyopita kulingana na chombo cha habari cha taifa.
Baada ya mkewe kufariki kutokana na matatizo ya kujifungua ,nduguze walimlazimisha mpenziwe kulipa ''Lobolo'', wakionya kwamba la sivyo hatozikwa.
Nduguze walimshutumu kijana huyo kwa kushindwa kuyafikia majukumu yake ikiwemo kutambulishwa kwa jamaa na ndugu za mwanamke huyo kabla ya janga hilo kutokea.
Ili kuhakikisha kuwa mazishi hayo yanafanyika, kijana huyo alilazimika kumnunulia nguo na viatu mkewe aliyefariki, kukubali kulipa zaidi ya dola 800 na kufanya haruasi mnamo tarehe 15 mwezi Disemba.
Nduguye kijana huyo Irmao do Jovem alielezea matatizo yao.
''Tulijaribu kuchangisha fedha walizotaka, lakini tuliweza kuchangisha dola 178 pekee.Hivyobasi ilibidi kuweka ahadi ya kulipa fedha zilizosalia siku ya harusi''.
Huku ikiwa familia ya kijana huyo imekubali kulipa,walishutumu tabia ya familia ya mwanamke huyo.
Hatahivyo, ni utamaduni miongoni mwa makabila mengi nchini Mozambique hususan iwapo mwanamume anaamua kuishi na mwanamke bila kufuatilia utamaduni wa kumuoa mwanamke huyo.
Via>BBC
Social Plugin