Mwenyekiti wa Chama Cha Waendesha Pikipiki maarufu bodaboda manispaa ya Shinyanga Jacob Paul (36) amejiua kwa kujinyonga kwa kutumia waya wa simu chumbani kwake katika mtaa wa Mwinamila kata ya Ngokolo katika manispaa ya Shinyanga.
Tukio hilo limetokea leo Jumamosi June 10,2017 mchana.
Tukio hili limetokea siku tano tu baada ya kutokea vurugu kati ya waendesha bodaboda na polisi baada ya mwendesha bodaboda mwenzao kufariki baada ya kukamatwa na askari wa usalama barabarani
Jacob Paul enzi za uhai wake
Social Plugin