Kambi ya Watoto na Vijana “Ariel Camp” iliyoandaliwa na shirika la Ariel Glaser Pediatric Aids Healthcare Initiative (AGPAHI) linalojihusisha na mapambano dhidi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) na Ukimwi nchini Tanzania iliyoanza June 19,2017 jijini Mwanza, imefungwa leo Ijumaa June 23,2017.
Kambi hiyo ilikutanisha watoto na vijana 50,walezi 11 walioambatana nao kutoka mikoa ya Shinyanga,Mwanza na Geita.
Miongoni mwa mambo waliyojifunza katika kambi hiyo iliyodumu kwa muda wa siku tano, ni pamoja na masuala ya lishe,ufuasi mzuri wa dawa,stadi za maisha,unyanyapaa na ubaguzi,haki na wajibu wa watoto pamoja na elimu ya afya ya ujana na makuzi.
Washiriki wa kambi hiyo pia walitembelea makumbusho ya Wasukuma ya Bujora na kufanya michezo mbalimbali nje ya darasa yenye kuashiria umoja,ushirikiano,upendo na kujenga mtazamo chanya kwenye maisha yao.
Akizungumza wakati wa kufunga kambi ya Ariel jijini Mwanza,mgeni rasmi,Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Dk. Silas Wambura,aliwataka watoto na vijana hao kuwa mabalozi wazuri wanaporudi nyumbani huku akiwasihi kuzingatia masomo na kanuni za afya ili kufikia malengo yao ya kimaisha.
Aidha, Dk. Wambura alisema serikali inatambua kazi nzuri inayofanywa na shirika la AGPAHI katika sekta ya afya na kwamba serikali itaendelea kushirikiana nao ili watanzania wengi zaidi waweze kunufaika na huduma zinazotolewa na shirika hilo hususani katika mapambano dhidi ya Virusi vya Ukimwi na Ukimwi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Miradi AGPAHI, Dk. Safila Telatela alisema takribani watoto na vijana 400 wameshapata fursa ya kushiriki Kambi ya Ariel tangu shirika hilo lilipoanzishwa mwaka 2011,ambapo washiriki hutoka kwenye klabu za vijana na watoto kwenye mikoa ambayo AGPAHI inafanya kazi zake.
“Mshiriki wa kambi lazima awe mwanachama wa klabu za vijana na watoto,lakini kwa mikoa hii mipya (Mwanza,Geita,Tanga na Mara),shirika liliamua kuwachukua vijana,watoto na walezi kushiriki kwenye kambi ndipo baadae uanze mchakato wa kuunda klabu/vikundi ili kutoa huduma za kisaikolojia kwa watoto”,aliongeza Dk. Telatela.
“Hii ni kambi ya nane tangu kuanza kwa shirika letu ,tulianza kufanya kazi katika mikoa ya Shinyanga na Simiyu,na kuanzia mwezi Oktoba mwaka 2016,tuliongeza mikoa minne ya Mwanza,Tanga,Geita na Mara hivyo kufikisha idadi ya mikoa sita ambako tunafanya kazi”,alieleza Dk. Telatela.
Katika hatua nyingine alisema shirika la AGPAHI linatekeleza majukumu yake kwa hisani ya Watu wa Marekani kupitia shirika la Centres for Disease Control and Preventation (CDC),mfuko wa kusaidia Watoto wenye VVU kwa hisani ya Watu wa Uingereza (CIFF) na Shirika la Development Aid From People to People (ADPP - Mozambique).
ANGALIA PICHA ZA MATUKIO WAKATI WA KUFUNGA KAMBI YA ARIEL MWAKA 2017 JIJINI MWANZA.
Washiriki wa Kambi ya Ariel 2017 wakiandamana kuelekea ukumbini wakati wa kufunga kambi hiyo leo Ijumaa June 23,2017 katika Hoteli ya Lesa Garden jijini Mwanza.
Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa jamii AGPAHI mkoa wa Mwanza, Cecilia Yona akitambulisha washiriki wa kambi ya Ariel kwa mgeni rasmi wakati wa kufunga kambi hiyo.
Mgeni rasmi ambaye ni Kaimu Mganga Mkuu wa mkoa wa Mwanza,Dk. Silas Wambura akitoa hotuba wakati wa kufunga kambi ya Ariel mwaka 2017.
Dk.Wambura akizungumza wakati wa kufunga kambi ya Ariel.Wa kwanza kulia ni Mratibu wa Miradi AGPAHI mkoa wa Mwanza, Olympia Laswai akifuatiwa na Mkurugenzi wa Miradi AGPAHI, Dk. Safila Telatela.Wa kwanza kushoto ni Mratibu wa Miradi AGPAHI mkoa wa Shinyanga,Dk. Gastor Njau akifuatiwa na Mratibu wa Ukimwi mkoa wa Geita Dk. Joseph Odero.
Watoto na vijana wakinyoosha mikono juu baada ya kuulizwa na Dk. Wambura kama wamefurahia kambi ya Ariel.
Mkurugenzi wa Miradi AGPAHI, Dk. Safila Telatela akizungumza wakati wa kufunga kambi ya Ariel jijini Mwanza. Alisema watoto na vijana walioshiriki kambi ya Ariel ni wale walioko kwenye umri balehe (miaka 10 - 17).
Washiriki wa kambi ya Ariel wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea.
Mkurugenzi wa Miradi AGPAHI, Dk. Safila Telatela akizungumza wakati wa kufunga kambi ya Ariel.
Watoto na vijana wakiimba na kucheza wimbo mbele ya mgeni rasmi,Dk. Silas Wambura.
Vijana wakicheza muziki.
Mtoto akionesha vazi la ubunifu kwa kutumia magazeti alilolitengeneza akiwa kambini baada ya kufundishwa somo la stadi za maisha.
Mtoto akielezea jinsi alivyofurahishwa na mambo mbalimbali akiwa kambini.
Mtoto akitoa ushuhuda wa mambo aliyojifunza akiwa kambini.
Vijana wakionesha igizo kuhusu ugonjwa wa Ukimwi.
Keki maalum kwa ajili ya washiriki wa kambi ya Ariel mwaka 2017.
Mgeni rasmi,Dk. Silas Wambura,Mkurugenzi wa Miradi AGPAHI, Dk. Safila Telatela na watoto walioshiriki Kambi ya Ariel wakikata keki.
Mgeni rasmi / Kaimu Mganga Mkuu wa mkoa wa Mwanza,Dk. Silas Wambura akimlisha keki mtoto.
Mtoto akimlisha keki mgeni rasmi Dk. Silas Wambura.
Mkurugenzi wa Miradi AGPAHI, Dk. Safila Telatela akilishwa keki na mtoto.
Muelimisha rika Mahene James kutoka Mwanza akishikana mkono na Kaimu Mganga Mkuu wa mkoa wa Mwanza,Dk. Silas Wambura wakati akipokea cheti cha ushiriki wa kambi ya Ariel.
Mtumishi wa afya kutoka mkoa wa Shinyanga aliyeambatana na watoto na vijana kutoka Shinyanga,Glory Assey akishikana mkono na Mkurugenzi wa Miradi AGPAHI, Dk. Safila Telatela baada ya kupokea zawadi ya cheti cha ushiriki wa kambi ya Ariel.
Mtumishi wa afya kutoka mkoani Geita Awipu Piniel akipokea zawadi ya cheti cha ushiriki wa kambi ya Ariel.
Kaimu Mganga Mkuu wa mkoa wa Mwanza,Dk. Silas Wambura akiangalia michoro ya miti ya maisha iliyochorwa na watoto na vijana walioshiriki kambi ya Ariel wakielezea kwa ufupi mambo wanayoyapenda katika maisha yao.
Kulia ni Kaimu Mganga Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Dk. Silas Wambura akiendelea kuangalia michoro ya miti ya maisha ya washiriki wa kambi ya Ariel. Kushoto ni Mratibu wa Ukimwi mkoa wa Geita, Dk. Joseph Odero akiangalia michoro hiyo.
Kijana akimwelezea Kaimu Mganga Mkuu wa mkoa wa Mwanza,Dk. Silas Wambura kuhusu mti wake wa maisha aliochora kuhusu historia yake ya maisha.
Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa Jamii AGPAHI mkoa wa Geita,Richard Kambarangwe akimwelezea mgeni rasmi,Dk. Wambura kuhusu shindano la 'Mkali Wao' ambapo washiriki hushindanishwa katika masuala mbalimbali mfano kujiamini,ucheshi,usikivu, utulivu,uchezaji mzuri wa muziki,kujibu maswali vizuri,uongozi mzuri,kutunza muda,nidhamu na utii na uchangamfu kambini na mshindi anayepatikana hupigwa picha katika bango hilo.
Picha ya pamoja: Mgeni rasmi na washiriki wa kambi ya Ariel.
Picha ya pamoja: Mgeni rasmi na wafanyakazi wa AGPAHI.
Picha ya pamoja: Mgeni rasmi na watumishi wa afya waliombatana na watoto na vijana kutoka mikoa ya Shinyanga,Mwanza na Geita.
Watumishi wa afya waliombatana na watoto na vijana kutoka mikoa ya Shinyanga,Mwanza na Geita wakiwa katika picha ya pamoja.
Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog
Bofya <<HAPA>> KUONA PICHA WATOTO NA VIJANA WA ARIEL CAMP 2017 WAKITEMBELEA MAKUMBUSHO YA KISUKUMA BUJORA MWANZA
Bofya <<HAPA>> KUONA PICHA WAKATI WA KUFUNGA KAMBI YA ARIEL JIJINI MWANZA
Bofya <<HAPA>> KUONA PICHA WATOTO NA VIJANA WA ARIEL CAMP 2017 WAKITEMBELEA MAKUMBUSHO YA KISUKUMA BUJORA MWANZA
Bofya <<HAPA>> KUONA PICHA WAKATI WA KUFUNGA KAMBI YA ARIEL JIJINI MWANZA