Mwili wa Shabiki maarufu wa timu ya Yanga Ally Mohamed almaarufu kwa jina la Ally Yanga aliyefariki dunia juzi katika ajali ya gari aina ya Rav4 eneo la kijiji cha Chipogoro wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma umezikwa leo katika makaburi ya Nguzo Nane mjini Shinyanga.
Mbali na kuwa mshabiki wa Yanga Ally Yanga pia alikuwa mkereketwa wa Mwenge wa Uhuru alikutwa na mauti akiwa katika gari la kampuni ya Faidika ambalo lilikuwa kwenye shughuli zake za promosheni na siyo kwamba alikuwa kwenye msafara wa Mwenge kama inavyoenezwa.
Ally alizaliwa mkoani Shinyanga Machi 1, mwaka 1984 katika familia ya watoto sita, kabla ya umauti wake alikuwa anaishi Yombo Vituka, Dar es Salaam.
Picha za Ally Yanga enzi za uhai wake
Mwili wa marehemu Ally Yanga ukiwa umebebwa kwa ajili ya mazishi katika makaburi ya Nguzo Nane Mjini Shinyanga leo Ijumaa June 22,2017.Picha zote na Marco Maduhu-Malunde1 blog
Mwili wa Marehemu Ally Yanga ukizikwa kwenye makaburi ya Nguzo Nane mjini Shinyanga
Awali kabla ya mazishi,Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Makusanya akiombea mwili wa marehemu Ally Yanga
Naibu katibu mkuu CCM bara Rodrick Mpogolo akitoa salamu za pole kwa niaba ya Mwenyekiti wa CCM taifa ambaye ni Rais John Pombe Magufuli
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack akitoa salamu za pole kwa niaba ya serikali
Naibu kartbu mkuu CCM bara Rodrick Mpogolo akisaini kitabu cha rambirambi nyumbani kwa Marehemu Ally Yanga Stendi ya Mabasi ya wilaya mjini Shinyanga
Mkuu wa Wilaya Josephine Matiro( wa tatu kutoka kulia) , akifuatiwa na mkuu wa Mkoa wa Shinyanga wakiwa msibani
Wananchi,wapenzi wa mpira wa miguu na viongozi wa serikali ,wabunge wakiwa kwenye maombolezo nyumbani kwao na marehemu Ally Yanga mjini Shinyanga
Wananchi wakiwa msibani
Picha zote na Marco Maduhu-Malunde1 blog