Rais John Magufuli jana alikutana na wajumbe wa kamati zilizofanya uchunguzi wa mchanga wa madini katika makontena 277 yaliyozuiwa bandarini.
Taarifa iliyotumwa na Kurugenzi ya Habari na Mawasiliano ya Ikulu jana Jumatano ilisema Rais amewapongeza wajumbe hao kwa kazi nzuri waliyoifanya.
Kamati hizo moja iliyoongozwa na Profesa Abdulkarim Mruma, ambaye timu yake ilichunguza kiasi cha madini kilicho kwenye mchanga huo na ya Profesa Nehemia Osoro iliyochunguza masuala ya kisheria kuhusu mchanga huo.
Rais Magufuli alisema timu hiyo imefanya kazi nzuri na yenye maslahi makubwa kwa Taifa na kwamba Serikali itahakikisha inafanyia kazi taarifa zilizotolewa na kamati hizo.