RAIS MAGUFULI : NIMECHOKA KUWALISHA WAFUNGWA,NATAKA WAKALIME ILI WAOGOPE KUFUNGWA

Rais John Magufuli amesema ni vizuri magereza yakawa na maeneo mengi ili wafungwa walime na wajue maana ya kufungwa ni nini.

Ameyasema hayo leo (alhamisi) wakati akizungumza wilayani Bagamoyo katika ziara yake ya siku tatu, mkoani Pwani.

 “Nimechoka kuwalisha wafungwa, mtu afungwe halafu anunuliwe chakula. Nimeshatoa maagizo, wafungwa hawa wakalime ili waogope kufungwa,” amesema na kuongeza;

“Wakajifunze kulima, wajue kufungwa ni kufungwa na neno kufungwa ni kufungwa kweli. Tukianza kuwapunguzia maeneo magereza, mnataka wakalime wapi?” amehoji.

Rais amesema, hiyo ndiyo sababu ya kutunza maeneo ya magereza ili yatumike kwa uzalishaji mali.

 Ameongeza kuwa ni vizuri wahalifu wakatumia nguvu kama walizotumia kuiba, ili wakalime.

“Huko magereza wafanye kazi, bila kujali vyeo walivyokuwa navyo, umaarufu wao na wakafanye kazi,” amesema

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم