SERIKALI YAZUIA USAFIRISHAJI MADINI WA MOJA KWA MOJA KUTOKA MGODINI


Serikali imesema haitaruhusu usafirishaji wa madini moja kwa moja kutoka mgodini na kupelekwa nje ya nchi.


Hayo yameelezwa jana Alhamisi na Waziri wa Fedha na Mipango, Phillip Mpango wakati akiwasilisha hotuba ya bajeti kwa mwaka 2017/18.


Badala yake kutakuwa na viwanja maalumu vya kimataifa katika bandari, migodini na madini hayo yatathibitishwa na kupewa kibali kabla ya kusafirishwa nje.


“Kibali hicho kitatozwa ada ya asilimia moja ya thamani ya madini hayo,” amesema.


Amesema Serikali itatangaza rasmi tarehe rasmi ya kuanza kwa ada hiyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post