Matamshi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kuhusu wanafunzi wanaopata ujauzito kutoendelea na masomo yamezua gumzo kubwa na mijadala mbalimbali ndani na nje ya nchi.
Shirika la wanawake barani Afrika limemtaka Rais Magufuli kuomba msamaha kutokana na matamshi yake aliyoyatoa akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Pwani kuwa mwanafunzi atakayepata ujauzito katika utawala wake hataweza kuendelea na masomo.
Hata hivyo, katika sheria iliyopitishwa mwaka 2002 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu suala la mtoto wa kike kupata ujauzito akiwa shule inaruhusu kufukuzwa shule na kifungo cha miaka 30 kwa yule aliyesababisha ujauzito huo.