Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TANESCO YAWAOMBA RADHI WATUMIAJI WA UMEME WILAYA YA KAHAMA


SHIRIKA LA UMEME TANZANIA

KUOMBA RADHI KWA KUKOSEKANA UMEME BAADHI YA MAENEO WILAYANI KAHAMA

Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) linawaomba radhi wateja wake wa Isaka, Kagongwa na maeneo yanayozunguka kutokana na kukosekana kwa huduma ya umeme kuanzia Jana tarehe 24/06/2017 saa 08:53 Mchana mpaka leo tarehe 25/06/2017 .

SABABU
Kutokana na hitilafu iliojitokeza kwenye laini ya Tinde/Kagongwa inayohudumia maeneo hayo na kusababisha kukosekana kwa huduma. 


MAENEO YANAYOATHIRIKA 
Ni maeneo yote kuanzia Isaka hadi Kagongwa 

UTATUZI

Mafundi wetu wapo kwenye laini wanaendelea na jitihada za kutambua hitilafu hiyo iliyosababisha ukosefu wa huduma ili kuweza kurebisha tatizo na kurejesha huduma mapema iwezekanavyo. 

Uongozi unaomba radhi Kwa usumbufu wowote unaoendelea kujitokeza.


Imetolewa na:

Ofisi ya Uhusiano na Huduma kwa Wateja-TANESCO Shinyanga.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com