ZITTO KABWE AUNGANA NA WADAU WA HABARI KUPINGA SERIKALI KUFUNGIA GAZETI LA MAWIO

Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto kabwe amepinga vikali hatua ya kufungiwa kwa gazeti la MAWIO na kudai kuwa hatua hiyo inawanyima Wananchi mawazo mbadala.

==>Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Zitto ameandika yafuatayo;

“Uamuzi wa kufungia gazeti la Mawio unapaswa kulaaniwa na kila mwanademokrasia. Uhusika wa Marais wastaafu kwenye mikataba ya madini umesemwa na Rais Magufuli Mwenyewe sio Mawio.

"Hakuna mkataba ulioingiwa bila Baraza la Mawaziri kuidhinisha. Kitendo cha Kamati ya Rais kutuhumu Mawaziri wa zamani mbele ya Rais Magufuli na yeye Mwenyewe Rais Magufuli kusema hatapona mtu ilikuwa ni dhahiri kuwa Rais anawachimba watangulizi wake.

"Kwa sisi tuliofundishwa lugha ya Uongozi tuling’amua mapema kuwa Rais Magufuli alikuwa anawatuhumu wenzake. Hivyo Gazeti la Mawio lilitafsiri tu maelezo ya Rais. Kitendo cha Rais kuonya kuwa Marais wastaafu waachwe ilikuwa ni KUJISEMESHA tu na kufungia gazeti la Mawio ni ‘ panick ‘ ya Rais Magufuli baada ya kuwasema watangulizi wake.

"Kila wakati Rais analia kuhujumiwa na kutaka kuombewa; Adui wa Magufuli ni Magufuli mwenyewe.

"Serikali ifungulie Gazeti la Mawio mara moja bila masharti kwani kulifungia ni kuwanyima Watanzania mawazo mbadala kuhusu mambo ya hovyo yanayoendelea nchini kwetu.
na kumalizia kwa hashtag ya #PressFreedom #UhuruWaHabari.”

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم