Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ZITTO KABWE: LEO NINAONA VITA DHIDI YA UFISADI INA MAANA KUBWA

Mbunge wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amemsifu Rais Dkt Magufuli kwa jitihada zake za kupambana na rushwa ambapo amesema kwa muda wote, leo ameona kuwa vita ya ufisadi ina maana kubwa.

Zitto ameyasema hayo jana kupitia ukurasa wake wa Twitter ambao aliandika jumbe kadhaa kupongeza jitihada hizo za Rais Magufuli ambapo katika moja ya jumbe zake alisema kuwa, kukamatwa kwa watuhumiwa hao wa sakata la Tegeta Escrow ni moja ya hatua kubwa sana za Rais Magufuli dhidi ya rushwa.

Zitto alisema kuwa licha ya kuwa amekuwa akimpinga Rais Magufuli katika mambo mbalimbali na ataendelea kumpinga, lakini katika hili la kukamatwa kwa James Rugemarila na Harbinder Sethi anamuunga mkono na kumpongeza sana.

Hapa chini ni jumbe za Zitto alizoandika kupitia ukurasa wake wa Twitter;


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com