ACACIA YAKUBALI KUILIPA SERIKALI MRABAHA WA ASILIMIA 6 KWA MUJIBU WA SHERIA MPYA

Kufuatia mabadiliko yaliyofanywa na Bunge katika sheria za usimamizi wa rasilimali nchini, ongezeko la mrabaha unaotarajiwa kulipwa serikali uliongezeka kutoka katika asilimia 4 iliyokuwa katika sheria za zamani.

Katika kuonyesha kukubaliana na mabadiliko hayo, Kampuni ya uchimbaji madini nchini ya Acacia imekubali kuilipa serikali mrabaha wa asilimia 6 unaoendana na sheria mpya zilizoanza kutumika mwezi huu mwanzoni baada ya kusainiwa na Rais Julai 5.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo leo inaeleza kuwa, ili kuepuka mkanganyiko au mvurugano zaidi kwenye kazi zao katika siku za usoni, watatimiza matakwa yanayohitajika katika ongezeko la mrabaha wa katika madini ya dhahabu, fedha na shaba la asilimia 6

Isome taarifa ya ACACIA hapo chini


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم