Mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Mwesigwa Mberwa (23),amekutwa amefariki dunia katika chumba namba 38 kwenye nyumba ya kulala wageni (guest house) iitwayo Msukuma, huko kitongoji cha usalama wilaya ya kipolisi Mlandizi - Pwani.
Kamanda wa polisi mkoani Pwani (ACP) Jonathan Shana ,amesema mfanyakazi wa nyumba hiyo ya kulala wageni Kulekwa Kulwa ,aligundua kutokea kwa tukio hilo saa mbili usiku jana .
"Alipoona imeingia siku ya nne bila ya kumuona mteja wake akitoka nje tangu aingie kwenye nyumba hiyo ya wageni tangu July 19 mwaka huu, ndipo alipotia shaka. Polisi walilazimika kuvunja mlango wa chumba na kumkuta Mwesigwa akiwa ameshafariki dunia," alisema ACP Jonathan Shana
Alisema mwili wa marehemu haukuwa na jeraha lolote na maiti imehifadhiwa hospital ya rufaa ya Mkoa ya Tumbi kwa ajili ya uchunguzi kisha utakabidhiwa kwa ndugu zake kwa mazishi .
Social Plugin