Mwanamme aliyejulikana kwa jina la Adam Joseph (30) ameuawa kwa kuchomwa kisu na ndugu yake aliyetajwa kwa jina la Benjamin Zakaria (22) kwa kile kilichotajwa kuwa ni deni la gunia moja la alizeti alilokuwa anadaiwa na ndugu yake huyo.
Joseph ambaye ni mjomba wa Benjamini Zakaria aliuawa katika tukio lililotokea usiku wa kuamkia jana Jumamosi kwenye kilabu cha pombe za kienyeji katika kijiji cha Ninga, wilayani Kalambo mkoani Rukwa.
Ofisa Mtendaji wa kijiji hicho, Yohana Kawea alisema ndugu hao walionekana wakibishana kwa muda, ndipo Zakaria alichomoa kisu na kumchoma nacho Joseph ambaye alifariki dunia papo hapo.
Alidai kuwa baada ya kumuua, alitokomea kusikojulikana na uongozi wa kijiji baada ya kupata taarifa za mauaji hayo, ulipeleka taarifa polisi kwa hatua zaidi.
Chanzo_
Social Plugin