Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

CHADEMA KUTOA TAMKO LEO

Kamati Kuu ya CHADEMA imekutana kwa siku mbili, tarehe 29 hadi 30 Julai, 2017 katika Hotel ya Double Tree, jijini Dar es Salaam kujadili hali ya siasa nchini pamoja na ukandamizwaji wa demokrasia .


Taarifa iliyotolewa jana na Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje, John Mrema inasema kwamba katika mambo ambayo Kamati Kuu imejadili ni pamoja na kamata kamata inayoendelea kufanywa na vyombo vya dola dhidi ya viongozi, wanachama na wafuasi wa CHADEMA maeneo mbalimbali nchi nzima.


Hata hivyo kikao hicho kilijadili na kufikia maazimio na hatua za kuchukua katika ajenda ambapo ni pamoja na kuporomoka kwa uchumi na hali ngumu ya maisha kwa watanzania, ambapo taarifa kamili juu ya maadhimio hayo na hatua zitakazochukuliwa na chama itatolewa leo Jumatatu tarehe 31 Julai 2017, kwenye kikao na waandishi wa habari kitakachofanyika jijini Dar es salaam.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com