Meneja wa Chapa ya Coca-Cola nchini Tanzania, Sia-Louise Shayo akizungumza na umati wa wasambazaji na mawakala wa soda ya Coca-Cola jijini Mwanza wakati wa hafla maalumu ya uzinduzi wa kinywaji kipya cha ‘Coca-Cola Bila Sukari’. Uzinduzi wa soda hii mpya umefanyika katika kiwanda cha Nyanza Bottlers mkoani Mwanza, ambapo pia baadaye utafanyika katika mikoa ya Dar es Salaam na Mbeya.
****
Kampuni ya Coca-Cola leo imezindua katika soko la Mwanza na kanda ya ziwa kwa ujumla, soda mpya ya “Coca-Cola Bila Sukari”. Uzinduzi wa soda hii mpya umefanyika katika kiwanda cha Nyanza Bottlers mkoani Mwanza, ambapo pia baadaye utafanyika katika mikoa Dar es Salaam na Mbeya ambapo awali ulifanyika mjini Moshi .
Soda mpya ya ‘Coca-Cola Bila Sukari’ ladha yake imeboreshwa zaidi kutokana na soda isiyo na sukari iliyokuwa inatengenezwa hapo awali ya Coca-Cola Zero ambapo soda mpya ladha yake inashabihiana na soda ya Coca-Cola asilia lakini haina sukari kabisa.
Tangia mwaka 2006 wakati soda ya Coke Zero imeingia kwenye masoko, kampuni ya Coca-Cola imekuwa ikifanya jitihada kuhakikisha inatengeneza soda mpya ya Coca-Cola isiyo na sukari lakini yenye ladha sambamba na Coca-Cola asilia na imefanikiwa kuja na soda mpya ya ‘Coca-Cola Bila Sukari’ kinywaji ambacho kitawezesha watumiaji wa Coca-Cola kuipata kwa ladha asilia hata kama watachagua kuipata isiyotengenezwa kwa sukari.
“Soda ya Coca-Cola Zero ina ladha nzuri pia, lakini pamoja na ubora wake timu ya Coca-Cola imekuwa ikifanyia kazi kuhakikisha inapatikana soda isiyo na sukari lakini yenye ladha inayoshabiana na Coca-Cola asilia”. Alisema Meneja Mauzo Mwandamizi wa Nyanza Bottlers, Deus Kadico.
Kadico aliongeza kuwa; “Ubunifu wa wataalamu wetu umewezesha kupatikana soda mpya ya ‘Coca Cola Bila Sukari’ ambayo inatoa wigo kwa wateja kuwa na chaguo la kupata kinywaji cha Coca-Cola kwa radha asilia kwa kadri wanavyotaka,ikiwa na ladha ya sukari ama isiyo na sukari”.
Pamoja na hayo, Kadico alisisitiza kuwa lengo kubwa ni kuhakikisha watumiaji wa soda ya Coca-Cola wanafurahia ladha yake halisi na asilia wanapokunywa soda yenye sukari au ‘Coca-Cola Bila Sukari’.
Soda za ‘Coca Cola Bila Sukari’ zimeanza kuwa kwenye soko la Tanzania kuanzia mwezi uliopita katika sehemu zote zinapouzwa soda na bei yake ni sawa na soda aina nyingine zote zinazotengenezwa na kusambazwa na kampuni ya Coca-Cola.