Mkuu wa Wilaya ya Urambo, Angelina Kwinga, akizungumza na maofisa Ugani wa wilaya hiyo wakati akifungua mafunzo ya siku moja kwa maofisa ugani kutoka kata zote na vijiji vya wilaya hiyo wilayani humo leo.
Mkurugenzi wa Halmshauri hiyo, Margareth Nakainga, akizungumza katika mafunzo hayo.
Picha ya pamoja kati ya Viongozi wa Wilaya ya Urambo,Watafiti pamoja na Maafisa ugani wa Wilaya hiyo.
*****
Mkuu wa Wilaya ya Urambo Angelina Kwingwa amewaomba watafiti wa kilimo toka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia(COSTECH) pamoja na Kituo cha Utafiti Ukiriguru wawape elimu nzuri ya kutosha katika kilimo cha zao la Pamba Maafisa Ugani wa wilaya yake ili waweze kulima kilimo hicho na kiwe chenye tija kwao.
Mkuu huyo wa wilaya aliyasema hayo wakati akifungua kifungua mafunzo ya siku moja kwa maofisa ugani kutoka kata zote na vijiji vya wilaya hiyo wilayani humo leo, yaliyolenga kukumbushana namna ya kulima kilimo cha kisasa na chenye tija kwa jamii ya sasa.
Angelina alisema pamoja na kwamba wilaya yake inalima zao kubwa la tumbaku lakini bado wanahitaji kuwa na zao la pamba pia lina manufaa kwao.
“Tunaomba watafiti mtusaidie kufundisha hawa maafisa ugani kulima zao hilo la pamba,japo wao wanalima lakini bado hatujafanya vizuri hivyo tunahitaji maafisa hao wapate mafunzo katika zao hili ili tuanze kulima na tufanikiwe kama wilaya nyingine”,alisema Angelina.
Aidha Mkuu huyo wa Wilaya aliwaomba maafisa ugani kufanyia kazi mafunzo waliyopewa katika sehemu zao husika ili yaweze kuzaa matunda kwao na kuboresha mazao ambayo wanalima sasa.
"Lakini pia niwaombe maafisa ugani kuchukua fursa hii na kuelewa unakwenda kupambana vipi katika kituo chako cha kazi ili kuanza kuleta mafaniko katika wilaya yetu na kuanza kuwa na kilimo cha kisasa,na kama tusipoona matokeo tutajua nyinyi ndiyo mtakuwa na matatizo na siyo wakulima",aliongezea Angelina.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa halmashauri ya Urambo Magreth Nakaingwa alibainisha kuwa ulimaji wa zao moja kama vile wao wanavyotegemea Tumbaku kumesababisha wakulima wengi kukosa namna ya kujikimu kimaisha kutokana na soko la tumbaku kushuka kwa kasi.
“Uchumi wa wilaya ya Urambo unategemea zaidi zao la tumbaku na msimu huu wa mavuno changamoto ambayo wakulima wamekutanayo ni kwamba masoko yameenda polepole kwanza yamechelewa kuanza lakini hadi sasa wakulima wa tumbaku hawajauza tumbaku katika maghala yao”alisema Magreth.
“Kutokana na hali hiyo wakulima wengi wamekosa fedha ambapo imewaathiri sana na sasa wanataka wakulima hao kujikita katika mazao mengine ya biashara ili waweze kuwa na njia nyingine ya kujipatia kipato”,alisema Magreth.
Hata hivyo Tume ya Taifa ya Sayansi (costech ) kupitia Jukwaa la baiteknolojia nchini (OFAB)imesema itaendelea kutoa mafunzo kwa maafisa ugani katika wilaya na mikoa mbalimbali lengo likiwa ni kufanya kilimo kiwe cha kisasa ili kufikia azma ya serikali ya awamu ya Tano ifikapo 2025 kuwa Tanzania ya viwanda.
Na Hellen Isdory - Urambo
Social Plugin