GARI LAUA WAPANDA VESPA WAWILI HUKO UNGUJA

WATU wawili waliokuwa wakitumia pikipiki ya magurudumu mawili maarufu kama Vespa, wamefariki dunia baada ya kugongwa na gari aina ya Hino eneo la Bungi Wilaya ya Kati Unguja.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja, Juma Sadi aliwataja watu hao kuwa ni Salami Khamis (26) aliyekuwa akiendesha Vespa hiyo yenye namba za usajili Z 633 akiwa amembeba Is-haka Kingwaba (27) walipogongwa na gari ya aina ya Hino na kufariki papo hapo.

Akifafanua zaidi, Sadi alisema vijana hao walikuwa wakiendesha Vespa ambao ni maarufu kwa jina la ‘T one’ walikuwa wakiendesha vespa hiyo kwa mwendo kasi na walikuwa wakikata kona na ndipo walipokumbana na gari ya Hino uso kwa uso na kugongwa na kufariki hapo hapo.

Kamanda sadi alisema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa Vespa hiyo. “Hawa vijana walipata ajali wakati wakijaribu kukata kona kwa mwendo wa kasi na ndipo walipopata ajali hiyo ambayo huyu dereva alikanyagwa kichwa,” alisema.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم