Wote wanaofatilia soka mnajua kwamba Mkuu wa kitengo cha Habari wa Simba SC Haji S. Manara alipewa kifungo kama adhabu na TFF siku zaidi ya 70 zilizopita lakini leo imekuja habari mpya kuhusu kifungo hicho.
Habari yenyewe ni kwamba Haji Manara ameachiwa huru na kamati ya nidhamu ya TFF na sasa ataendelea na majukumu yake kama kawaida.
Simba SC imethibitisha taarifa hiyo kwa kusema “Kamati ya nidhamu ya TFF imemuachia huru mkuu wa kitengo cha Habari wa klabu ya Simba Haji Manara sasa kuendelea na majukumu yake kama kawaida.”
Social Plugin