Matokeo ya kidato cha sita kwa mwaka 2017 yametoka leo Jumamosi, Julai 15 huku shule ya Wasichana ya Feza Girls ikiibuka kinara kwa watahiniwa wake 67 kufaulu kwa kupata daraja la kwanza na la pili.
Shule nyingine zilizoibuka kidedea katika matokeo hayo ni Marian Boys, iliyoshika nafasi ya pili, Kisimiri (Arusha) imeshika nafasi ya tatu na Ahmes (Pwani) imeshika nafasi ya nne.
Shule nyingine ni Marian Girls (Pwani) iliyoshika nafasi ya tano, Mzumbe (Morogoro) nafasi ya sita, St Marry Mazinde Juu (Tanga) nafasi ya saba, Tabora Boys (Tabora) nafasi ya nane, Feza BOYS (Dar es Salaam) nafasi ya tisa na Kibaha ya Pwani iliyoshika namba kumi.
Poleni kwa usumbufu mliopata siku ya leo wa kuhangaika kutafuta Link sahihi inayoweza kukuonesha matokeo ya kidato cha sita 2017 yaliyotangazwa leo .Hii hapa chini ni link sahihi inayofungua matokeo hayo bila matatizo.Bonyeza link hii hapa chini.
Social Plugin