Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

JAJI WA MAHAKAMA KUU ALIYEJIUZULU AFARIKI DUNIA

Aliyekuwa Jaji wa Mahakama Kuu ambaye amejiuzulu  hivi karibuni, Upendo Msuya amefariki leo Julai 19 baada ya kuugua kwa muda mrefu ugonjwa wa kiharusi.

Mjomba wa marehemu, Niva Mbaga amethibitisha tarifa hizi na kusema kwamba marehemu amefariki akiwa Hospitali ya Kairuki alipokuwa amelazwa.

Amesema kwamba shughuli za mazishi zinafanyika nyumbani kwa marehemu Tegeta jijini Dar es Salaam.

“Amesumbuliwa kwa muda mrefu na ugonjwa wa kiharusi hivyo akawa anapelekwa hospitali na kurudi nyumbani zaidi ya miezi mitatu sasa na leo hii amefariki dunia’’ amesema Mbaga

Amesema marehemu ameacha watoto wanne.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com