Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

JESHI LA POLISI LAWASAKA WATUHUMIWA 16 WA MAUAJI KIBITI

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Eng. Hamad Yussuf Masauni ametangaza kuwa, Jeshi la Polisi linawasaka watuhumiwa 16 wa mauaji ambayo yamekuwa yakiendelea kufanyika katika maeneo ya Kibiti, Mkuranga na Rufiji mkoani Pwani kwa muda mrefu sasa.


Masauni amesema jeshi jilo litatumia nguvu zote inazoweza kuweza kukomesha mauaji hayo ili wakazi wa eneo hilo waweze kuishi kwa amani na kurudi kwenye maisha yao ya kila siku.


Akitaja baadhi ya majina ya watuhumiwa hao wanaotafutwa alisema ni pamoja na Hassan Haruna Kyakalewa Shujaa, kutoka Ikwiriri mwenye umri kati ya miaka 25-35. Mwingine ni Omari Abdallah Matimbwa.


Wengine wanaosakwa na jeshi hilo ni, Anafi Rashid Kapera kutoka Kibiti mwenye miaka kati ya 25-30 mrefu wa wastani, mwenye uso wa mviringo na wa mwisho ni, Faraji Ismail Nangalava kutoka Kibiti mwenye kati ya miaka 25-35.


Masauni aliyasema hayo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema Jeshi la Polisi lina picha za watuhumiwa wote wanaotafutwa.


Aidha Jeshi la Polisi lilisema kuwa, zawadi nono itatolewa kwa watakaofanikisha kukamatwa kwa wahalifu hao.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com