Makazi ya Naibu Rais wa Kenya Willium Ruto
****
Washambuliaji ambao bado idadi yao kujulikana wameshambulia makazi ya vijijini ya Naibu Rais wa Kenya Willium Ruto mjini Sugoi.
Namna walivyoingia makazi hayo ambayo yana ulinzi mkali ni kama filamu iliyopangwa ikapangika vizuri, kwa mujibu wa vyanzo vya habari nchini Kenya washambuliaji hao walitafuta namna ya kuingia katika lango kuu la jumba hilo wakashindwa ikabidi watumie akili ya kuhadaa wana usalama waliopo eneo hilo.
Ili wasishtukiwe kirahisi walimtuma mmoja wao kwenda getini akiwa amebeba bidhaa kadhaa za nguo akiijifanya ni muuzaji wa nguo hizo, kwa kuwa alikuwa ameshika nguo hizo wanausalama walimpuuza wakijua ni muuzaji wa nguo. Mtu huyo alisimama getini na kumwita afisa usalama aliyekuwa getini na silaha na kumwambia anauza nguo.
Mara baada ya mwanausalama huyo kufika jamaa huyo aliyejifanya muuza nguo alimkamata na kumnyang'anya silaha yake akamfyatulia risasi mbili moja begani na nyingine kichwani. Papo hapo washambuliaji waliojihami kwa silaha walifika langoni hapo na kuingia ndani huku wakifyatua risasi ovyo ndani ya nyumba hiyo.
Vikosi vya usalama vinaendelea na operesheni ya kupambana na washambuliaji hao huku ikiwa bado kujulikana sababu ya mashambulisi hayo katika nyumba ya kiongozi mkubwa katika nchi.
Imebainika kuwa watu hao walikuwa wakimsubiri Naibu wa Rais Willium Ruto atkitoka na gari kwenda katika kampeni ili wamshambulie, lakini baada ya kusubiri kwa muda mrefu bila kiongozi huyo kutoka wakaamua kuingia kwa staili hiyo wakiwa na lengo la kumsaka Willium Ruto.
Kwa bahati nzuri kiongozi huyo aliamua kuondoka kwa helkopta kutokea katika makazi yake na kuelekea katika eneo la mkutano wa kampeni, hii ikawa bahati kubwa kwa kiongozi huyo wa Kenya kukumbwa na masaibu ambayo yumkini yangeweza hata kuchukua uhai wake.
Vikosi vya usalama viliwasili dakika 15 baada ya mashambulizi hayo kuanza na kuzingira nyumba hiyo ambapo milio ya risasi iliendelea kusikika kwa zaidi ya saa mbili. Hadi habari hii inaadikwa na kuingizwa mtandaoni habari zinasema kuwa milio ya risasi kati ya maafisa usalama na washambuliaji hao ilikuwa inaendelea kusikika.
Tukio hilo linatokea wakati Naibu Rais Wilium Ruto akiwa katika kampeni zake za lala salama. Tukio hili linazidisha hofu kuhusiana na hali ya usalama wakati huu wa uchaguzi ukikaribia.