MAAFISA UGANI WILAYA YA NYANG'WALE WATAKIWA KUTUMIA NAFASI ZAO VIZURI KUNUFAISHA WAKULIMA


Mkuu wa wilaya ya Nyang'wale Hamimu Gwiyama akifungua mafunzo kwa maafisa ugani 27 kutoka wilaya hiyo yaliyoandaliwa na Tume ya taifa ya sayansi na teknolojia COSTECH kupitia Jukwaa la bioteknolojia la Kilimo(OFAB)- Picha na Hellen Isdory
Mtaribu wa OFAB Tanzania Philbert Nyinondi akizungumza na wagani lengo ya mafunzo hayo.
Picha ya pamoja kati ya mkuu wa wilaya ya Nyang'wale pamoja sambana na watafiti toka Costech pamoja na maafisa ugano 53 wa wilaya hiyo.

****

Maafisa ugani wilaya ya Nyang’wale Mkoani Geita wametakiwa kutumia nafasi zao vizuri kwa wakulima ili kuwafanya kulima kilimo cha kisasa ambacho kina tija katika jamii kwa ujumla.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa wilaya ya Nyang’wale Hamimu Gwiyama wakati akifungua mafunzo kwa maafisa ugani 27 kutoka wilaya hiyo yaliyoandaliwa na Tume ya taifa ya sayansi na teknolojia COSTECH kupitia Jukwaa la bioteknolojia la Kilimo(OFAB) yenye lengo la kuwakumbusha wataalamu hao nafasi yao katika kilimo ili kutoa mbinu kwa wakulima kuwa na kilimo cha kisasa hasa katika mazao ya mizizi.

Hamimu alisema kwamba kuna fursa nyingi katika Mkoa huo hasa zinazo husu kilimo kama wagani hao wataweza kufanyia kazi ipasavyo mafunzo hayo watakayopewa na wataalamu basi wakulima wataanza kuneemeka.

“Zipo fursa nyingi katika wilaya hiyo ambapo upo uwezekano wa kulima mazo ya Pamba,Dengu,Mahindi kama mafunzo hayo mtafanyia kazi vizuri naamini njaa katika wilaya yangu ni historia”,alisema Hamimu

Kwa upande wake Mratibu wa OFAB Tanzania Philbert Nyinondi alisema wapo katika kutekeleza sera ya nchi ya uchumi wa viwanda hivyo wameona ni vyema kutoa elimu namna ya kupata kilimo cha kisasa na chenye tija ambacho kitainua pato la Taifa.

“Kikubwa kilichotuleta ni kuweka makundi haya makubwa mawili kati ya wagani na watafiti ili kwa pamoja waweze kujua namna ya kutataua changamoto ya kilimo ili kwenda katika uchumi wa viwanda”,alisema Nyinondi.

Hata hivyo baadhi wa wagani katika wilaya hiyo wamesifu mafunzo hayo na kusema kwamba fursa za kilimo zilizopo katika wilaya hiyo zitaenda vizuri kama bajeti wakitengewa na kuweza kuwa na mashamba darasa kwa wakulima ambapo itakuwa rahisi kwao kutoa elimu vizuri kwa wakulima.
Na Hellen Isdory- Nyang'wale

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم