MWALIMU mmoja wa kiume, mwenye umri wa miaka 39, amelazwa hospitalini nchini Zimbabwe baada ya genge moja ya wanawake watatu kumteka, kumlewesha kwa dawa na kufanya naye ngono kabla ya kumtekeleza kando ya barabara.
Mtu huyo kutoka sehemu ya Makoni, Wilaya ya Chitungwiza, nchini humo aliachwa akiwa na majeraha na michubuko kwenye sehemu zake za siri ambapo madaktari wa hospitali ya Waza waligundua alikuwa pia amenyanyaswa kingono.
Polisi wanawatafuta wanawake watatu wanaodaiwa kuwa sehemu ya “genge la manii” ambapo huwanasa watu wanaokutwa barabarani peke yao au wasafiri na kuwashambulia ili kuchukua manii yao (mbegu za kiume) kwa ajili ya kuyatumia kwa kile kiitwacho “bahati njema”.
Mtu huyo aliiambia polisi kwamba wakati akisubiri basi kituoni Julai 2 mwaka huu, alipewa lifti katika gari dogo la rangi ya bluu aina ya BMW likiwa na namba za usajili za Afrika Kusini lililokuwa linaendeshwa na mwanamme.
Ndani ya gari hilo kulikuwa na wanawake watatu. Baada ya hapo, alisema alipewa kinywaji cha kawaida akiwa ndani ya gari hilo na baadaye kukinywa alijisikia kizunguzungu na kulala.
Social Plugin