MBUNGE WA CHADEMA AACHIWA KWA DHAMANA YA SHILINGI MILIONI 10


Mbunge wa Kawe, Halima Mdee ameachiwa kwa dhamana baada ya kusota rumande kwa siku sita.


Mdee ameachiwa leo Julai 10, kwa dhamana ya Sh10 milioni na wadhamini wawili, baada ya kusomewa shitaka la kutumia lugha chafu na Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa.


Mbunge huyo, alikamatwa Julai 4 kwa amri ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi aliyeamuru awekwe mahabusu kwa saa 48.


Hapi alidai, Mdee amemkashifu Rais na ndicho chanzo cha kutupwa rumande kwa saa hizo.


Wakili Katuga amedai kwamba, mnamo July 3, mwaka huu katika Ofisi za CHADEMA makao makuu, alimtukana Rais Magufuli kwa kumwambia anaongea ovyo ovyo, anatakiwa afunge break.

Baaada ya kusomewa shtaka hilo Halima Mdee alikana kosa hilo na kesi imeahirishwa kutokana na upelelezi kutokamilika mpaka tarehe 7 mwezi wa 8 mwaka huu ambapo kesi itatajwa tena.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم