Mfanyabiashara maarufu nchini anayemiliki hoteli za kifahari jijini Arusha, Maleu Mrema amefariki dunia nchini Afrika Kusini alipokuwa akipatiwa matababu.
Kwa mujibu wa familia ya marehemu, Maleu ambaye anamiliki Hoteli za Impala, Naura, Ngurdoto zilizopo jijini Arusha, wamesema ndugu yao alifia Afrika Kusini na kwamba taarifa zaidi kuhusu msiba huo zitatolewa leo.
Familia wamesema hadi sasa hawajapata taarifa rasmi kutoka hospitalini hapo kuelezea chanzo cha kifo cha mpendwa wao.
Mrema alipelekwa Afrika Kusini mwezi Juni mwaka huu baada ya kusumbuliwa na matatizo ya kiafya.
The Impala Group of Hotels inajumuisha:
1) Impala hotel (Arusha)
2) Impala hotel (Moshi)
3) Ngurdoto Mountain Lodge (Arusha)
4) Naura Springs Hotel (Arusha)
5) Impala shuttle Services (Arusha)
6) The Classic Tours & Travels
Social Plugin