Polisi wakiongea na watu nje ya tukio
Mwanaume mmoja amekamatwa kwa madai kuwa aling'ata na kukata kidole cha mtu mwingine wakati was sherehe ya harusi mjini Sydney Australia.
Mvamizi huyo mwenye umri wa miaka 42 aliingia katika sherehe moja ya harusi siku ya Jumamosi usiku na kujaribu kuiba mkoba.
Wakati wageni walipomkabili, mvutano ukatokea ambapo mwanamume huyo aling'ata kidole cha mtu mwingine.
Kidole kilichong'atwa hakiwezi kuokolewa, kwa mujibu wa vyombo vya habari.
Mwanamume aliyeumia alipelekwa hospitalini ambapo alitibiwa na kuruhusiwa kwenda nyumbani.
Hizo hazikuwa ghasia za mwisho usiku huo kwa kuwa polisi walilazimika kuvunja mapigano yaliyotokea nje ya klabu.
Via>>>BBC
Social Plugin