Nyani azima umeme kwa karibu saa 6 nchini Zamabia
Nyani alivuruga mitambo ya umeme katika mji wa Livingstone nchini Zambia na kukata umeme kwa karibu watu 50,000.
Nyani huyo alifanikiwa kuingia katika kituo cha umeme siku ya Jumapili, na kuvuruga mitambo yenye umeme inayosambaza umeme kuenda maeneo ya Kusini na magharibi mwa Zambia kwa mujibu wa kampuni ya umeme nchini humo Zesco.
Alisema kuwa wakaazi 28,000 wa Livingstone na watu wengine 22,000 wa eneo hilo walibaki kabisa bila umeme kwa zaidi ya saa sita wakati ukarabati ulikuwa ukiendelea.
"Nyani huyo alipigwa na umeme lakini kutokana na maumbile yake ya kimazingira alipata tu majeraha mabaya ya moto. Kama angekuwa binadamu angekufa." alisema Kapata.
Kapata alisema kuwa kampuni hiyo imeomba msamaha wateja wake kwa hasara waliyoipata.
Mji wa Livingstone ni maarugu kwa wanyama pori kama nyani na ndovu wanaotoka mbuga iliyo karibu.
Social Plugin