Picha : WADAU WA ELIMU WAKUTANA KUJADILI SEKTA YA ELIMU MKOA WA SHINYANGA



 Leo Jumatano Julai 19,2017 wadau wa elimu mkoa wa Shinyanga wamekutana kujadili masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya elimu mkoani Shinyanga. 



Kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga pamoja na mambo mengine kililenga kujadili mafanikio na changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya elimu mkoani Shinyanga.

Kikao hicho kimeongozwa na Katibu Tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela.

Miongoni mwa mambo yaliyoleta mjadala mrefu zaidi ni pamoja na suala la mimba kwa wanafunzi na uhaba wa vyoo na madawati katika shule.

Akitoa taarifa katika kikao hicho,Afisa Elimu mkoa wa Shinyanga Mohammed Kahundi alisema hivi sasa mkoa una jumla ya madarasa ya elimu ya awali 601 na kati ya hayo,madarasa 562 yapo katika shule za msingi za serikali na shule za awali za watu binafsi,mashirika ya kidini na taasisi binafsi.

Kahundi alisema pia kuna jumla ya shule za msingi 600 kati ya hizo,shule 562 ni za serikali na shule 38 zinamilikiwa na watu binafsi na mashirika ya kidini na taasisi binafsi.

 Aliongeza kuwa shule za sekondari zipo 139 kati ya hizo 116 ni za serikali/wananchi na 23 ni za mashirika ya dini,taasisi binafsi na watu binafsi.

"Idadi ya shule za sekondari za kidato cha tano na sita zimeongezeka kutoka shule moja mwaka 2005 hadi kufikia 8 mwaka 2017,shule hizo ni Shinyanga Sekondari,Old Shinyanga,Mwendakulima,Kishapu,Tinde wasichana,Dakama,Abdulhahim Busoka na Mwalimu Nyerere,lakini pia zipo shule mbili za watu binafsi ambazo ni Buluba na Don Bosco Didia",alisema.

 Alisema wananchi mkoa wa Shinyanga wanaendelea kunufaika na elimu ya juu kupitia Chuo Kikuu Huria cha Tanzania na Chuo Kikuu cha Ushirika Kampasi ya Kizumbi na tayari vyuo hivyo vina wanachuo wanaoendelea na masomo katika kozi mbalimbali.

"Mkoa una vyumba vya madarasa 3,744,nyumba za walimu 1,243,stoo 222 na matundu ya vyoo 4522,mahitaji yaliyopo ni vyumba vya madarasa 7,961,nyumba za walimu 7,622,matundu ya vyoo 13,987 na stoo 569,hivyo kuna upungufu wa vyumba vya madarasa 3,732,nyumba za walimu 6,379,matundu ya vyoo 9,445 na stoo 347",alieleza Kahundi.

Aidha Kahundi alisema mkoa una mapungufu ya madawati 127921,yaliyop ni 1117313 hivyo kuna upungufu wa madawati 9864 sawa na asilimia 7.7 ambapo upungufu huo umetokana na idadi kubwa ya wanafunzi 89,578 walioandikishwa darasa la kwanza mwaka 2017 wakati waliomaliza darasa la saba mwaka 2016 walikuwa 25,523.

Kwa upande wake katibu tawala mkoa wa Shinyanga Albert Msovela alisema changamoto katika sekta ya elimu zitatuliwa endapo wadau wote wa elimu watashirikiana katika kuzikabili changamoto hizo.


Mwandishi wetu Kadama Malunde,yupo katika kikao hicho ametuletea picha za matukio yaliyojiri katika kikao hicho..Tazama Hapa chini
Afisa Elimu mkoa wa Shinyanga Mohammed Kahundi akizungumza wakati wa kikao hicho ambapo alisema idadi ya wanafunzi na usajili wa shule mpya umeongezeka mkoani Shinyanga wakati wa mfumo wa elimu bila malipo.

Katibu tawala mkoa wa Shinyanga,Albert Msovela akizungumza ukumbini ambapo alisema ili kumaliza changamoto zilizopo katika sekta ya elimu ni vyema wadau wote wakashiriki katika kutatua changamoto hizo.
Meza kuu wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini
Wadau wa elimu wakiwa ukumbini.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Nyabaganga Talaba akichangia hoja wakati wa kikao hicho.
Wakurugenzi wa Halmashauri za wilaya mkoani Shinyanga wakiwa ukumbini
Meza kuu wakifuatilia kilichokuwa kinajiri ukumbini
Wadau wakiwa ukumbini
Kikao kinaendelea
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu,Boniface Butondo akichangia hoja wakati wa kikao hicho.
Mchungaji Joram wa kanisa la Waadventista Wasabato mjini Shinyanga akichangia hoja ukumbini.
Kikao kinaendelea
Mdau akichangia hoja ukumbini
Kushoto ni mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Ngassa Mboje na Diwani wa kata ya Kambarage mjini Shinyanga,Hassan Mwendapole wakisoma nyaraka muhimu wakati wa kikao hicho.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Msalala,Simon Berege akichangia hoja ukumbini
Wa kwanza kushoto ni Padre Joachim Mahona kutoka kanisa katoliki Jimbo la Shinyanga na Mwenyekiti wa makanisa ya kipentekoste mkoa wa Shinyanga Mchungaji Elias Madoshi kutoka kanisa la FPCT wakisoma taarifa muhimu ukumbini.
Kikao kinaendelea..
Afisa Elimu mkoa wa Shinyanga Mohammed Kahundi akisoma taarifa wakati wa kikao hicho
Kushoto ni katibu tawala wilaya ya Shinyanga,Boniface Chambi akitafakari jambo ukumbini

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم