Mama mzazi wa Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’, Halima Hassan aliyefariki dunia Alhamisi hii asubuhi, baada ya kuugua kwa wiki kadhaa na kulazwa hospitali amezikwa jana Ijumaa katika Kitongoji cha Munyonyo, Kampala nchini Uganda.
Kifo cha mama Zari ambaye alizaliwa Mei 15, 1959, kimekuja ikiwa ni takribani miezi miwili tu tangu mkwe wake, Ivan Semwanga, aliyeaga dunia Mei 25 mwaka huu huko Steve Biko Academic Hospital nchini Pretoria, Afrika Kusini.
Diamond ambaye ni mpenzi wa Zari, alisafiri na team yake ya WCB kwa ajili ya kushiriki mazishi hayo. Angalia picha za mazishi.
Social Plugin