Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

RAIS MAGUFULI AKATAA MIALIKO ZAIDI YA 60 KWENDA NJE YA NCHI KUINYOOSHA TANZANIA KWANZA


Rais John Magufuli amesema amepata mialiko zaidi ya 60 kwenda nje ya nchi baada ya kuwa Rais lakini ameikataa kwa sababu anataka kuishughulikia Tanzania kwanza.


Ameyasema hayo jana (Jumanne Julai 4,2017) wakati akihutubia wakazi wa Sengerema katika uzinduzi wa mradi wa maji Sengerema.


Rais Magufuli amesema hana haja ya kwenda nje ya nchi kwa sababu bado ana mzigo mkubwa wa kumaliza ufisadi.


“Niende nje kufanya nini wakati ntaenda tu nikishastaafu, nataka nimalize kwanza haya ya hapa ndani,” alisema.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com