Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Prof. Florens D.A.M Luoga kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) leo hii na kuanza kazi mara moja.
Awali nafasi hiyo ilikuwa chini ya Bw. Bernard Mchomvu ambaye bodi yake ilivunjwa na uteuzi wake kutenguliwa mnamo Novemba 20 mwaka 2016.
Pamoja na hayo, Prof. Florens D.A.M Luoga ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Taaluma).